Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni akituhumiwa kuua shangazi yake

93727 Mauaji+pic Mbaroni akituhumiwa kuua shangazi yake

Thu, 30 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Njombe. Mkazi wa mjini Makambako mkoani Njombe, anashikiliwa kwa tuhuma za kumpiga na kumsababishia kifo shangazi yake, Elina Mwinuka (18) kwa madai ya kuchelewa kurudi nyumbani.

Kamanda wa polisi mkoani Njombe, Hamis Issah alisema mtuhumiwa alikamatwa juzi.

“Mtuhumiwa alimtuma Elina (marehemu) dukani lakini binti huyo alichelewa kurudi na aliporejea nyumbani, inaelezwa aliaanza kumshushia kipigo kichwani na sehemu tofauti za mwili wake,” alidai Kamanda Issa.

Alisema kipigo hicho kilimsababishia Elina uvimbe kichwani na maumivu, kisha kufariki dunia akipelekwa Hospitali ya Mji Makambako.

Issah alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo kwa uchunguzi na taratibu nyingine kabla ya kukabidhiwa ndugu.

Alisema baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Pia Soma

Advertisement
Wakati huohuo, Kamanda Issah alisema wanawashikilia watu 14 kwa tuhuma za wizi wa mali maeneo tofauti.

Alisema miongoni mwa vitu walivyokamatwa navyo ni televisheni, pikipiki, redio, kompyuta, magodoro na sufuria.

Alisema katika msako huo, pikipiki saba zilipatikana na kati hizo mbili zilikuwa zimefunguliwa na kuuzwa kama spea.

Chanzo: mwananchi.co.tz