Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni akidaiwa kumuua baba yake mzazi

Mbaroni Mbaroni akidaiwa kumuua baba yake mzazi

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

POLISI mkoani Mbeya wamemkamata kijana aliyefahamika kwa jina la Humphrey Kihali (25) akituhumiwa kumuua baba yake mzazi, Francis Kihali (50).

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Antony Mkwawa alisema Septemba 10, mwaka huu saa 10: 45 za jioni katika eneo la Ilemi, Humphrey alimvizia baba yake akiwa chumbani kwake akampiga kwa kutumia ubao.

Kamanda Mkwawa alisema baada ya hapo Kihali alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na aliaga dunia jana saa moja na nusu asubuhi.

Alisema ingawa uchunguzi wa awali umeonesha mtuhumiwa ana tatizo la akili, uchunguzi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuate.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live