Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbaroni akidaiwa kumkata kichwa, viganja, nyeti mtoto wa kufikia

Pingu Law Mbaroni akidaiwa kumkata kichwa, viganja, nyeti mtoto wa kufikia

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia, Erick Julias (39) mkazi wa Mlimba wilayani Kilombero kwa tuhuma za kumuua na kumtenganisha kichwa pamoja na viungo vingine mtoto wake wa kufikia, Johnson Ngonyani (6).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 4, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema pamoja na mtuhumiwa huyo kumkata kichwa, pia alimkata seheme za siri (uume na korodani) na viganja vyote viwili.

Kamanda Mkama amesema mtuhumiwa alitenda ukatili huo Juni 1 mwaka huu majira ya usiku katika Kitongoji cha Kigamboni, Kijiji cha Mwembeni, Mlimba Wilaya ya Kilombero.

Amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kutokana na taarifa za raia wema na baada ya kuhojiwa Polisi amekiri kufanya mauaji hayo na ametoa ushirikiano kwa kuonyesha sehemu alikoficha viungo hivyo.

Mwingine amuua mumewe

Wakati huohuo, Polisi wamemkamata Jovina Mwakiyee (33) mkazi wa Kijiji cha Mang'ula A kwa tuhuma za kula njama na kumuua mume wake Christian Tungaraza (39), mwalimu mkuu Shule ya Msingi Signal.

"Tukio hili limetokea Juni 1, mwaka huu majira ya usiku huko katika Kitongoji cha Gendeni, Kijiji cha Mang'ula A, Wilaya ya Kilombero ambapo mtuhumiwa huyo amedaiwa kula njama zilizofanikisha kuuawa kwa mumewe," amesema Kamanda Mkama.

Mkama amesema mwalimu huyo akiwa amelala na mtuhumiwa (mke wake) na watoto wao wawili, alivamiwa ndani na kuuawa kwa kupigwa na kitu butu kichwani.

Amesema polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwapata watuhumiwa wengine wanaodaiwa kushirikiana na mwanamke huyo.

Katika tukio jingine la mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Elly Kimaro (53) mkazi wa Arusha, Polisi wamewakamatwa Hassan Mbwambo (31), mganga wa kienyeji mkazi wa wilayani Same, Kilimanjaro na John Matunda (20), dereva wa bodaboda mkazi wa Dumila Wilaya ya Kilosa.

Wengine ni Boniface Mwendi (31), mkazi wa Kijiji cha Berega na Neema Mbwambo (32) mkazi wa Wilaya ya Moshi vijijini.

Kamanda Mkama amesema tukio hilo la mauaji ya mfanyabiashara huyo lilitokea Mei 26, 2024 saa mbili usiku, ambapo watuhumiwa wanadaiwa kumnyang’anya marehemu Sh20 milioni na kisha kumuua.

Kamanda Mkama amesema Kimaro alisafiri kutoka Arusha hadi Turiani mkoani Morogoro kufanya biashara ya madini akiwa na Hassan Mbwambo ambaye ni mmoja wa watuhumiwa.

"Baada ya kufika eneo la Turiani mtuhumiwa kwa kushirikiana na mwenzake Samwel Matunda wakiwa na pikipiki, walimteka hadi Kijiji cha Berega na kumyang'anyana fedha na kumtaka mume wa marehemu aongeze Sh5 milioni ili wamuachie mkewe," amesema Kamanda Mkama.

Alisema baada ya kupatiwa kiasi hicho cha fedha, walimuua mke na kuutelekeza mwili wake katika shamba la mbaazi hadi mwili huyo ulipoonekana na wasamaria wema.

Kufuatia matukio hayo ya mauaji hayo, Kamanda Mkama amewataka wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya wenza wao, kwani matukio mengi ya mauaji yamehusisha mapenzi, imani za kishirikina, tamaa ya mali na fedha pamoja na migogoro ya kifamilia.

Chanzo: Mwananchi