Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazungumzo vigogo Halotel DPP yafikia hatua za mwisho

HALOTEL.webp Mazungumzo vigogo Halotel DPP yafikia hatua za mwisho

Tue, 5 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo sita wa Kampuni ya Viettel Tanzania akiwamo Mkurugenzi wa Kampuni ya Halotel, Son Nguyen (46), umedai kuwa mazungumzo ya kukiri makosa kati ya washtakiwa hao na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) yamefikia hatua za mwisho.

Kadhalika Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai wanasubiri kibali kwa DPP ambaye yuko jijini Dodoma atakaporejea wataendelea kufuatilia.

Madai hayo yalitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati kesi hiyo ya uhujumu uchumi ikiwamo kuisababishia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), hasara na kutakatisha zaidi ya Sh. bilioni 75 ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa.

Wankyo alidai kesi hiyo imepangwa kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa utetezi Majura Magafu, alidai washtakiwa waliandika barua kwa DPP ya kutaka kukiri makosa yao mapema Aprili 21, mwaka huu.

Wankyo alijibu kwamba barua ya washtakiwa imepokelewa, tayari na majadiliano yameanza na wamekamilisha kwa kiasi kikubwa, kinachosubiriwa ni hati ya DPP ya kuipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuendelea na kesi hiyo.

"Mheshimiwa hakimu DPP yuko Dodoma hivyo akirudi tutaendelea kufuatilia, tunaiomba mahakama ipange kesi hii baada ya siku 14 au wakikamilisha kabla ya siku hizo washtakiwa watapelekwa mahakamani," alidai Wankyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live