Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakili wanne wajitosa kuwatetea waliotumwa na Afande

Mawakili Wanne Wajitosa Kuwatetea Waliotumwa Na Afande.png Mawakili wanne wajitosa kuwatetea waliotumwa na Afande

Wed, 21 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mawakili wanne wanaowatetea watuhumiwa wanne wakiwamo askari wa Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Magereza wamesema wanaimani haki itatendeka na itaonekana kutendeka dhidi ya wateja wao.

Watuhumiwa katika kesi hiyo ya ubakaji kwa kikundi na kumlawiti kwa binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam ni askari wa JWTZ MT.140105 Clinton Damas, askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Lord Lema na Nickson Jackson.

Kesi hiyo imeanza kusikilizwa leo Jumanne, Agosti 20, 2024 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma mbele ya Hakimu Mkuu Zabibu Mpangule na inatarajiwa kuendelea mfululizo hadi Ijumaa ya Agosti 23, 2024.

Watuhumiwa hao wanatetewa na mawakili wanne wakiongozwa na Godfrey Wasonga. Wengine ni Sadiki Omari, Boniventura Njeru na Meshaki Ngamando.

Baada ya kuahirishwa hadi kesho saa 4:00 asubuhi, Ngamando amesema upande wa Serikali imepeleka mashahidi watano lakini kutokana na muda wamemsikiliza shahidi mmoja.

Pia, amesema hawakumaliza kusikiliza na kumhoji baada ya askari magereza kueleza muda umeisha na walitaka kuwarudisha watuhumiwa mahabusu. Ngamando amewatoa hofu Watanzania kuwa haki itatendeka na itaonekana kutendeka hivyo wasiwe na wasiwasi kuhusu hilo.

"Wananchi na waandishi wa habari tuwe na utulivu tusikilize kesi...naimani kwamba haki itatendeka na siyo tu kutendekea bali itaonekana kuwa imetendeka," amesema Ngamando.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live