Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakili wakwamisha kesi ya vigogo Chadema

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikishindwa kuwasomea maelezo ya awali viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutokana na mawakili wao kuwa na kesi nyingine, imempa onyo mshtakiwa wa tano Ester Matiko.

Mawakili hao Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya walikuwa na kesi nyingine Mahakama Kuu.

Wakili aliyewakilisha upande wa utetezi, Hekima Mwesipu alidai kuwa Kibatala yuko Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Mtobesya yuko Mahakama Kuu Mtwara.

Baada ya maelezo hayo, wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi aliieleza mahakama kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH), lakini mawakili wao hawakufika.

Pia, alieleza kuwa mshtakiwa Matiko mara ya mwisho iliposikilizwa kesi hiyo hakutokea na mdhamini wake kueleza kuwa alikuwa na dharura, hivyo kumtaka atoe ufafanuzi wa kulichomsibu.

Katika maelezo yake Matiko alidai alipigiwa simu ya dharura na mwalimu anayemfundisha mwanaye kwenda shuleni Agosti mosi saa 4: usiku, baada ya kufika shule alikutaka mtoto wake akiumwa na kumpeleka hospitali alikopumzishwa kwa siku nne.

Hakimu Mashauri alimuonya Matiko kwa kutompa taarifa mdhamini wake na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13.

sababu za mdhamini wake kueleza kuwa alikwenda nchini Kenya, kutaka kujua alikwenda kufanya nini.

“Nakupa onyo mara nyingine uwe muwazi na mkweli iwe mara ya mwisho, siku nyingine unapaswa kumweleza mdhamini wako ni dharura gani imekupata,” alisema Mashauri na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni katibu mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji; naibu makatibu wakuu, Salum Mwalimu (Zanzibar) na John Mnyika (Bara).

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; mbunge wa Kawe, Halima Mdee na mbunge wa Bunda, Ester Matiko.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa 13.

Chanzo: mwananchi.co.tz