Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakala 10 wa ATCL waendelea kusota rumande

Mawakala 10 wa ATCL waendelea kusota rumande

Tue, 12 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wanaokabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Sh10,874,280 kwa lengo la kuwakatia watu tiketi za ndege za shirika hilo wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi kutokakamilika.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 97 /2018 ni Fabian Ishengoma(34), Adamu Kamara(27), Mlon Masubo(29), na Alexander Malongo(24),

Wengine ni Tunu Kiluvya (32), Jobu Mkumbwa(30), Mohamed Issa(38), Godfrey Mgomela, Absalom Nyusi na Janeth Lubega(24).

Wakili wa Serikali, Janeth Magoa amedai leo Jumanne Machi 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Wakili Magoa ameiomba Mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ambapo Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 26, 2019.

Wakili wa utetezi, Sharot Lupembe ameomba kuharakishwa upelelezi wa kesi hiyo kwa kuwa washtakiwa wako ndani. Washtakiwa wote wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la utakatishaji kutokuwa na dhamana.

Katika kesi ya msingi washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Machi 10 na Oktoba 9 mwaka 2018 wakiwa maeneo ya mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Mwanza walilisababishia shirika hilo hasara ya Sh10,874,280 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka lingine washtakiwa hao wanadaiwa  kati ya Machi 10 na Oktoba 9 mwaka 2018 wakiwa katika mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Mwanza walitumia njia ya udanganyifu kujipatia kiasi cha Sh10,874,280 kwa lengo la kuwakatia watu tiketi za ndege la shirika hilo.

Katika Shtaka la utakatishaji wa fedha washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Machi 10 na Oktoba 9 mwaka 2018 wakiwa katika mkoa wa Dar es Salaam na mkoa wa Mwanza walijipatia Sh10,874,280 mali ya shirika la ATCL huku wakijua ni kosa la kisheria.

Mawakala 10 wa ATCL waendelea kusota rumande



Chanzo: mwananchi.co.tz