Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mawakala 10 wa ATCL waendelea kusota rumande

41610 Atclpic Mawakala 10 wa ATCL waendelea kusota rumande

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mawakala 10 wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) wanaokabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Sh10,874,280 kwa lengo la kuwakatia watu tiketi za ndege za shirika hilo wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi kutokakamilika.

Washtakiwa katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 97 /2018 ni Fabian  Ishengoma (34), Adamu Kamara(27), Mlon  Masubo(29),  Alexander Malongo(24).

Wengine ni Tunu Kiluvya (32), Jobu Mkumbwa(30), Mohamed Issa (38), Godfrey Mgomela, Absalom Nyusi na Janeth Lubega(24).

Wakili wa Serikali, Janeth Magoa amedai leo Jumatano Februari 13, 2019  mbele ya hakimu mkazi mkuu, Salum Ally kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Wakili Magoa ameiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa na hakimu Ally ameahirisha hadi Februari 26, 2019.

Washtakiwa wote wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la utakatishaji kutokuwa na dhamana.

Katika kesi ya msingi washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Machi 10 na Oktoba 9, 2018 wakiwa maeneo ya Dar es Salaam na Mwanza walilisababishia shirika hilo hasara ya Sh10,874,280 huku wakijua kufanya hivyo ni kosa.

Katika shtaka lingine washtakiwa hao wanadaiwa  kati ya Machi10 na Oktoba 9, 2018 wakiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza walitumia njia ya udanganyifu kujipatia kiasi cha Sh10,874,280 kwa lengo la kuwakatia watu tiketi za ndege la shirika hilo .

Katika Shtaka la utakatishaji wa fedha washtakiwa wote kwa pamoja kati ya Machi10 na Oktoba 9, 2018 wakiwa katika mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza walijipatia Sh10,874,280 mali ya ATCL huku wakijua ni kosa la kisheria

Soma Zaidi: Mawakala ATCL waendelea kusota rumande



Chanzo: mwananchi.co.tz