Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matukio ya watoto kujipiga risasi

72223 Mwanafunzipic

Tue, 20 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Februari, 2019 Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lupanga manispaa ya Morogoro, Jasmine Ngoye (18) alijipiga risasi na kufariki, huku akimuachia ujumbe rafiki yake aliyekuwa akisoma naye darasa moja.Risasi hiyo ilipita katika koo na kufumua sehemu ya nyuma ya kichwa huku chanzo kikielezwa kuwa ni msongo wa mawazo.Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema muda mfupi baada ya tukio hilo, shemeji wa binti huyo, Profesa Hamisi Mahigi alijitokeza na kueleza kuwa bastola hiyo ni yake na anaimi-liki kihalali.Kamanda huyo alisema binti huyo aliacha ujumbe aliouandika katika kitabu chake cha kumbukumbu kabla ya kujipiga risasi, alimkabidhi rafiki yake aliyekuwa akisoma naye darasa moja.Julai, 2018, Mtoto wa miaka miwili katika jimbo la Texas nchini Marekani alijipiga risasi kwa kutu-mia bastola ya baba yake na kufariki dunia akiwa nyumbani kwao na wazazi wake.Polisi katika Jimbo la Texas walifanya uchunguzi kubaini ni kwa namna gani mtoto huyo anaweza akafanya tukio hilo na namna gani aliweza kuifikia bunduki hiyo mahari ilipokuwa huku wakitoa tahadhari kwa raia wanaomiliki bunduki kuwa makini katika uhifadhi.Mei, 2017, Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya upili ya Aga Khan nchini Kenya, alijipiga risasi kichwani na kufariki kwa kutumia bunduki ya baba yake.Kijana huyo Michael Kariuki, alikuwa peke yake nyumbani kwao wakati alipofanya tukio hilo.Mei, 2016, Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 18 nchini India alijipi-ga risasi kimakosa wakati akijaribu kujipiga picha ya ‘selfie’ akiwa na bastola ya baba yake.Hata hivyo kijana huyo hakufa papo hapo bali alikuwa na siku kad-haa za kutibiwa katika hospitali kuu ya Pathankot iliyoko katika jimbo la Punjab.Kijana huyo alikuwa ametoka shule muda mfupi na mashuhuda walieleza kuwa alichukua bastola ya babake iliyoidhinishwa na Seri-kali lakini kwa bahati mbaya akaji-piga risasi kichwani akitaka kupiga ‘selfie’ akiwa ameshika bastola kichwani.

Chanzo: mwananchi.co.tz