Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matukio 1361 ukatili wa kijinsia yaripotiwa Katavi

Bc085ea44b3237d01b71238f40a1e86e Matukio 1361 ukatili wa kijinsia yaripotiwa Katavi

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka huu 2022, Mkoa wa Katavi umepokea matukio 1361 yanayohusu ukatili wa kijinsia yakiwemo matukio 887 yanayohusu ukatili dhidi ya watoto.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, wakati akizungumza na wanahabari kuelekea kwenye maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani itakayofanyika Mei 15, 2022.

Amesema kuwa kwa mkoa wa Katavi matukio yanayoongoza katika takwimu hizo ni pamoja na ubakaji, ulawiti, kutelekeza familia, ajira za watoto, vipigo pamoja na mimba za utotoni.

"Niombe sana familia kutenga muda wa kukaa pamoja, kujadili mambo ya kifamilia, kufanya uamuzi na mipango ya pamoja,hii inajenga upendo na mshikamano ikiwa ni pamoja na kufahamu maendeleo ya watoto nyumbani hadi shuleni na kuwapeleka sehemu za ibada, ili kujenga jamii imara," amesema Mrindoko.

Amezitaka familia zote kutimiza wajibu wao katika suala zima la malezi, ili kuondokana na wimbi la familia zinazotelekezwa pamoja na watoto wa mtaani.

"Familia ikipata mahitaji muhimu chakula, malazi, mavazi, ulinzi na upendo, naamini kabisa mambo haya ya ukatili hayawezi kutokea," ameongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live