Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mateso! Mwanamke adai kuchomwa na pasi na mzazi mwenzake

Mateso A0001 Mateso! Mwanamke adai kuchomwa na pasi na mzazi mwenzake

Sun, 13 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni mateso na maumivu makali! Ndivyo unavyoweza kusema, unapokutana na Happyness Ringo (30), katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa kKilimanjaro Mawenzi, anapoendelea kupatiwa matibabu, baada kujeruhiwa kwa kuchomwa na pasi, kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake, na mtu anayedai kuwa ni mzazi mwenzie.

Akisimulia tukio hilo kwa chungu huku akibubujikwa na machozi, Happynes amesema kuwa alipatwa na mkasa huyo Agosti 5, mwaka huu, katika eneo la Nyiresi, Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, wakati alipokutana na mzazi mwenzie kwa ajili ya kuchukua nguo za mtoto.

Amesema awali aliishi pamoja na mwanaume huyo kama mume na mke, lakini waliachana baada ya kuwa na migogoro ya mara kwa mara, iliyosababisha yeye kupigwa na mwanaume huyo, jambo ambalo lilimfanya arudi kuishi kwa mama yake.

Amesema siku ya tukio, baba huyo alimpigia simu na kumtaka wakutane mjini, ili aweze kumpa nguo za mtoto, na kwamba kwa kuwa walikuwa wakiwasiliana kwa ajili ya mtoto, hakuona shida wala wasiwasi ya kukutana nae, na walipokutana ndipo alimfanyia ukatili huo.

Muunguzi ldara ya Upasuaji katika hospitali hiyo, Ladyness Moshi, amesema walimpokea Happyness Agosti 6, 2023; akitokea Hospitali ya Wilaya ya Hai, ambapo alikuwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amekiri kuokotwa kwa Happynes akiwa na majeraha mbalimbali, na kwamba anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Mawenzi, na kwamba undani zaidi wa tuko hilo, unaweza kupatikana mkoani Arusha ambako tukio liltokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live