Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Matatani wakikutwa na magunia ya mirungi

Mirungi Mirungiiii Matatani wakikutwa na magunia ya mirungi

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, limewakamata watu wawili wakituhumiwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi magunia sita na bunda 300 sawa na kilo 150 wakisafirisha, eneo la kijiji cha Ilkiushbour tarafa ya Makame.

Akizungumza jana Jumatatu Desemba 11,2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP George Katabazi amesema watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na bunda 300 sawa na kilo 150 zikiwa zimepakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruser yenye rangi nyeusi.

"Pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa Wilaya ya Hanang katika maafa ya mafuriko, Jeshi la Polisi Manyara bado tunaendelea na msako na operesheni mbalimbali ambapo Desemba 10, 2023 tulikamata watuhumiwa wawili wakisafirisha dawa za kulevya aina ya mirungi," amesema ACP Katabazi.

Kamanda Katabazi amewataja watuhumiwa Abdala Mohamed (53) na Hamidu Athuman (50) huku akisema walikutwa Kijiji cha Ilikushbour kata ya Makame wakisafirisha kwa gari hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live