Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maswali kibao shehena ya dhahabu

35148 PIC+DHAHABRU Tukio la kukamatwa kwa kilo 323.6 za dhahabu pamoja na Sh305 milioni

Tue, 8 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar/Mwanza. Tukio la kukamatwa kwa kilo 323.6 za dhahabu pamoja na Sh305 milioni zikisafirishwa kutoka mkoani Mwanza kwenda mkoa wa Geita limeacha maswali mengi.

Miongoni mwa maswali hayo yameulizwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alipokuwa akieleza kushangazwa kwake na jinsi watuhumiwa walivyosafirisha dhahabu hiyo kutoka Mwanza kwenda mkoani Geita, badala ya Geita kwenda Mwanza katika tukio ambalo Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko alisema ni ajabu kuona Watanzania wakiibia nchi yao.

“Suala hili linachanganya na kuibua maswali mengine ambayo majibu yake yatapatikana baada ya vyombo vya ulinzi na usalama kukamilisha uchunguzi wa awali. Naamini kufikia Jumatano tutakuwa na taarifa kamili,” alisema Mongella kwa simu jana.

“Watu wengi tumezoea kuona dhahabu ikisafirishwa kutoka Geita kuja Mwanza, sasa hii ya kusafirishwa kutoka Mwanza kwenda Geita ni jambo jipya linalohitaji uchunguzi makini.”

Kuhusu thamani ya dhahabu hiyo, mkuu huyo wa Mkoa alisema hayo ni miongoni mwa mambo yanayochunguzwa kwa sababu kunahitajika utaalamu kujua kiwango cha ubora kwanza.

Pamoja na kuchunguza uhalali wa shehena na fedha hizo, Mongella alisema vyombo vya ulinzi na usalama pia vinachunguza asili ya dhahabu hiyo na mtandao uliohusika.

“Siwezi kusema ilikuwa inatoroshwa kwenda nje ya nchi kupitia mipaka ya Geita. Hilo ni suala litakalojulikana baada ya uchunguzi kukamilika,” alisema akijibu taarifa kuwa shehena hiyo ilikuwa ivushwe kimagendo kwenda nje ya nchi.

Bila kutaja majina ya watuhumiwa, Mongella alisema mmoja mwenye asili ya Asia ni mkazi wa Mwanza wakati wengine wawili ni wenyeji wa Geita.

Katika maelezo yake, Biteko alisema Serikali ina mtandao unaosaidia upatikanaji wa taarifa za utoroshaji wa madini.

“Serikali inawatambua na inawaona kila mahali. Kwa sasa wamebakia wachache... Inasikitisha kuona mchimbaji mdogo analiibia Taifa lake wakati mipango ya Serikali ni kumwezesha mchimbaji wa ndani,” alisema.

Mkurugenzi Mkazi Kanda ya Afrika wa Shirika la Kufuatilia Usimamizi wa Rasilimali za Asili (NRGI), Silas Olang alisema changamoto iliyopo ni uadilifu kwa wasimamizi waliopewa dhamana na Serikali.

“Kuna wakaguzi wa migodi wanaopata taarifa za uzalishaji na usafirishaji wa madini, wamechimba kiasi gani, wame pata kiasi gani kwa hiyo hakuna kitu kingine zaidi ya uadilifu kwa wachimbaji na wasimamizi,” alisema.

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Madini na Nishati (NUMET), Nicomedes Kajungu alitaka mitandao ya utoroshaji idhibitiwe.



Chanzo: mwananchi.co.tz