Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashtaka matatu ya Tito Magoti na mwenzake, wakosa dhamana

89827 Magoti+pic Mashtaka matatu ya Tito Magoti na mwenzake, wakosa dhamana

Thu, 26 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mfanyakazi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Tanzania, Tito Magoti (26) na mtaalamu wa Tehama, Theodory Giyani (36), wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Magoti na Giyani, wote wakazi wa Tabata, Dar es Salaam wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumanne Desemba 24, 2019 na kusomewa mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh17milioni.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Janeth Mtega na jopo la mawakili wanne wa Serikali ya Tanzania.

Kabla ya kusomewa mashtaka hao, hakimu Mtega amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na Mahakama ya Kisutu kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai Magoti na Giyani, wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 137/2019.

Simon alidai katika shtaka la kwanza, Magoti na Giyani wanadaiwa kushiriki genge la uhalifu.

b2b2943b1c87b171483-text/javascript"> (adsbygoogle = window.adsbygoogle || []).push({}); Kosa hilo wanadaiwa kutenda, katika tarehe tofauti kati ya Februari mosi na Desemba 17, 2019 jijini Dar es Salaam katika maeneo mbalimbali ya ndani ya nchi, ambapo Magoti, Giyani na wenzao ambao hawajafikishwa mahakamani, kwa makusudi walishiriki makosa ya uhalifu ikiwa ni kumiliki programu za kompyuta iliyotengenezwa mahususi kwa ajili ya kufanya uhalifu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai katika shtaka la pili, washtakiwa hao na wenzao ambao bado hawajafikishwa mahakamani, wanadaiwa siku na eneo hilo, wanadaiwa kumiliki  programu za kompyuta kwa lengo la kutenda kosa la uhalifu.

Katika shtaka la tatu, ambalo ni kutakatisha fedha, Wakili wa Serikali Mkuu, Renatus Mkude, alidai Magoti na Giyani, wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Februari mosi na Desemba 17, 2019 katika Jiji la Dar es Salaam na maeneo mengine ndani ya nchi.

Wanashtakiwa hao wanadaiwa katika tarehe hizo, walijipatia Sh17.35 milioni wakati wakijua fedha hizo ni zao tangulizi la kushiriki genge la uhalifu.

Upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 7, 2020 itakapotajwa.

Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na shtaka la kutakatisha fedha linalowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz