Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashine haramu za kubeti zateketezwa

Collage (38) Mashine haramu za kubeti zateketezwa

Sat, 29 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board of Tanzania-GBT) imeteketeza mashine haramu za kuendeshea michezo ya kubahatisha (Slot Machines) zipatazo 300.

Sambamba na hilo watu Wanane (8) wako mikononi mwa vyombo vya kisheria wakihusishwa na mashine hizo.

Zoezi hilo lililoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa GBT Bw. James Mbalwe limefanyika Oktoba 28, 2022 kwenye eneo la kuteketeza vifaa vya kielektroniki lililoko Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

“Katika jitihada za kudhibiti waendeshaji haramu wa michezo ya kubahatisha GBT iliendesha operesheni maalum kwenye mikoa ya Pwani, Lindi, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Morogoro, Manyara na Songwe na kufanikiwa kukamata mashine hizo zenye thamani ya shilingi Milioni 300,” alifafanua Bw. Mbalwe.

Alisema mashine hizo zilikamatwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufanya biashara bila ya Leseni ya GBT, mashine kuingizwa nchini bila ya kufuata taratibu za kisheria, kufanya biashara kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi au hayajakaguliwa na kuthibitishwa na Bodi (GBT) pamoja na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live