Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mashahidi 26 kutoa ushaidi kesi dereva gari iliyoua sita

HUKUMU Mashahidi 26 kutoa ushaidi kesi dereva gari iliyoua sita

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashahidi 26 wanatarajiwa kuanza kutoa ushahidi wao dhidi ya dereva wa gari inayodaiwa kuwagonga wakimbia mchakamchaka eneo la Kiseke wilayani Ilemela mkoani Mwanza na kusababisha vifo vya watu sita na kujeruhi wengine tisa.

Katika kesi hiyo ya Trafiki namba 27/2023, mshtakiwa, Oswald Binamungu (39) anakabiliwa na shtaka lenye makosa 15 likiwemo la kuendesha gari kwa kasi na kusababisha vifo vya watu sita na kujeruhi wengine tisa kinyume na kifungu namba 40 (1), 63 (2) (a) na 27 (b) cha Sheria ya Usalama Barabarani namba 168 marejeo ya mwaka 2002.

Akimsomea mshtakiwa maelezo ya awali leo Agosti 10, 2023, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Amani Sumari, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Monica Mweli amesema Oswald aliwagonga kwa nyuma watu waliokuwa wanafanya mazoezi ya kukimbia mchakamchaka katika barabara ya Kiseke wilayani Ilemela mkoani humo.

‘’Ukiendesha gari kwa uzembe na mwendokasi, mshtakiwa uliwagonga kwa nyuma waliokuwa wanafanya mazoezi na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi tisa ambapo uchunguzi wa madaktari ulibaini kuwa marehemu walifariki baada kupata mivunjiko mwilini ,’’amesema Wakili Monica.

"Upande wa Jamhuri mbali na kuwa na mashahidi 26, tumejipanga kuwasilisha vielelezo 17 ambavyo ni ripoti za daktari sita, fomu namba tatu (PF3) tisa, ramani ya tukio na ripoti ya ukaguzi wa eneo la tukio," amesema Monica.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live