Kiongozi wa kundi moja hatari la dawa za kulevya nchini Colombia, Dairo Antonio Usuga amesafirishwa kwenda nchini Marekani ambako atafunguliwa mashtaka ikiwemo uingizaji nchini humo dawa za kulevya.
Usaga anadaiwa kuwa na wafuasi wapatao elfu sita ambao walikuwa wakifanya kazi chini yake baadhi yao wakiwa ni viongozi na watendaji wa kada mbalimbali nchini Colombia.
Rais Ivan Duque Marques wa Colombia amesema nchi yake haiwezi kuwa maficho ya makundi ya kihalifu ambayo yamekuwa yakidhoofisa hali ya amani na usalama kwa kufanya mauaji, utekaji nyara watu na ukatili mwingine na kusababisha wananchi kuishi kwa hofu.