Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Marehemu alikuwa akidandia treni" Kamanda Simiyu

RPC SIMIYU WEB 660x400 Maalim Seif akiri kupokea barua kutoka Serikali ya Mwinyi, ajibu

Sat, 21 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Galula Luhende (50), mkazi wa Malampaka, wilaya ya Maswa, mkoa wa Simiyu, amefariki dunia baada ya kugongwa na Treni usiku wa kuamkia leo Novemba 20, 2020.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao, amesema kuwa treni hiyo ilikuwa ikitokea Jijini Mwanza kwenda DSM na kwamba kabla ya ajali ilisimama Malampaka kupakia abiria.

“Marehemu alikuwa akidandia Treni hiyo iliyokuwa imeanza kuondoka, ndipo alipoteleza na kuanguka na kukanyagwa miguu” ACP Abwao.

“Marehemu huyo kabla ya kufariki, alikimbizwa Kituo cha Afya Malampaka na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya wilaya ya Maswa kwa matibabu” ACP Abwao

NABII BUSHIRI, UTAJIRI WA KUTISHA, MALI KUSHIKILIWA, ANA NDEGE, JUMBA LA KIFAHARI, MAGARI

Chanzo: millardayo.com