Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapipa 32 ya lami yakamatwa Bunda

LAMI3 Mapipa 32 ya lami yakamatwa Bunda

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: EATV

Jumla ya mapipa ya lami 32 yenye thamani ya zaidi shilingi milioni 30, yamekamatwa wilayani Bunda mkoani Mara baada ya kuweka mtego na kubaini wezi ambao wanaiba vifaa pamoja na malighafi zinazotumika katika ujenzi wa barabara ya Buramba Nyamswa inayojengwa na kampuni ya CRCC ya nchini China.

Akizungumza tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo Joshua Nassari, amesema tabia ya wizi wa malighafi zinazotumika katika ujenzi wa miradi umekuwa ni wa mara kwa mara jambo ambalo lilipelekea kufanya uchunguzi wa kina na kubaini uwepo wa mtandao ambao unafanya uhalofu katika mradi huo.

"Niliamua kufanya mwenyewe uchunguzi huu kwa kuwashirikisha watu wachache ndipo juzi tarehe 23 usiku nilipokuja hapa katika pori hili na kukuta wizi ukifanyika," amesema Nassari.  

Chanzo: EATV