Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mapenzi yaua mjamzito wa miezi sita

Panga Mke auwawa kwa kukatwa na Panga.

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Mkazi wa kata ya Malezi wilayani Handeni mkoani Tanga, Nassoro Mustapha anatuhumiwa kumuua mkewe kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali mwilini ikielezwa sababu ni wivu wa mapenzi, Tukio hilo limetokea katika mtaa wa Kwamaraho.

Dada wa marehemu, Rehema Hemed amesema wanahisi tukio hilo limetokana na wivu wa mapenzi kwa sababu wanandoa hao walikuwa na ugomvi na kwamba shemeji yake alikuja nyumbani wakiwa hawapo na kumshambulia mdogo wake.

"Nilikuwa kazini nikapata taarifa kwamba mdogo wangu amekatwa panga na mumewe, tulifika nyumbani na kumkuta amejeruhiwa mwili lakini alifariki tukiwa njiani kumpeleka hospitali, "amesema Rehema.

Rehema amesema ndugu yake amefariki akiwa ni ujauzito wa miezi sita au na ameacha mtoto wa miaka mitatu.

Diwani wa Malezi, Shabani Kitombo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa ni la pili katika mtaa huo mwaka huu.

"Nilivyoelezwa huyu binti amechalazwa mapanga maeneo ya shingoni na mumewe na chanzo cha ugomvi ndugu zake wanahisi ni sababu za mapenzi na mhusika anaendelea kutafutwa baada ya kukimbia, " amesema Kitombo.

Chanzo: Mwananchi