Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maombi dhamana ya wakili Madeleka kusikilizwa Aprili 29

Maombipic Data Wakili Peter Madeleka

Mon, 25 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maombi ya dhamana ya wakili wa kujitegemea, Peter Madeleka anayeshikiliwa na polisi, yametajwa leo, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Maombi hayo namba 16/ 2022, yalifunguliwa mahakamani hapo, Aprili 22, 2022 dhidi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania(DPP), Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam( ZCO).

Madeleka kupitia jopo la mawakili wake sita, wakiongozwa na Jebra Kambole waliwasilisha maombi hayo mahakamani hapo, akiomba mteja wake apewe dhamana, baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi, kwa siku sita sasa, bila kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo, maombi hayo yametajwa leo, Apili 25, 2022 mbele ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi anayesikilizwa shauri hiyo.

Awali, wakili Kambole ameieleza mahakama hiyo kuwa maombi hayo yamepangwa leo kwa ajili ya usikilizwaji na wapo tayari.

Kwa upande wa wajibu maombi, kupitia wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga alikiri kupokea maombi hayo na kuiomba Mahakama iwapatiwe muda zaidi kwa ajili ya kuyapitia ili waweze kujibu.

Advertisement “Tunakiri kupokea maombi, ambayo yalifunguliwa mahakamani hapa siku ya Ijumaa, April 22, 2022 saa 9:45 mchana, maombi haya yameletwa muda wa kazi ukiwa umeisha na hatukupata muda wa kuyapitia hadi leo hii, lakini taasisi zilizotajwa katika maombi haya ambazo ni IGP, DCI, ZCO zimehamishiwa Dodoma, hivyo tumeshindwa kuwasiliana nao kwa ajili ya kujibu maombi haya na kuandaa kiapo kinzani kwa leo,” amesema Katuga na kuongeza.

“Tumeona wenzetu wamewasilisha maombi yao kwa nyaraka ya usikilizwaji wa haraka, hivyo na sisi tunaona ni haki na subira kama tutaleta kiapo kinzani mahakamani hapa na tunahitaji kuwasiliasna na wenzetu ambao ni IGP, DCI na ZCO, hivyo kupitia sababu hizo tunaomba tupewe angalau wiki mbili, ili tuweze kujibu maombi haya.”

Hakimu Kyaruzi, baada ya kusikiliza hoja za pande zote amesema kuwa maombi hayo yaliitwa ajili ya kutajwa na kujua kama upande wa majibu maombi wamepewa nakala.

Kuhusu kupewa wiki mbili kwa wajibu maombi ili waweze kupitia na kujibu maombi hayo, hakimu Kyaruzi amesema kulingana maombi hayo kuwasilishwa kwa hati ya usikilizwaji wa haraka, inabidi yasikilizwe kwa haraka ili kutenda haki.

“Hivyo kwa nia ya kutenda haki, mahakama inaelekeza upande wa wajibu maombi   kuwasilisha kiapo kinzani Aprili 28, 2022 na maombi ya dhamana yatasikilizwa Aprili 29, 2022, saa 4:00 asubuhi,” amesema hakimu Kyaruzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live