Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maofisa wa polisi wanaodaiwa kuwapiga watendaji wa mamlaka ya kuzuia rushwa lawamani

41667 Maafisapic Maofisa wa polisi wanaodaiwa kuwapiga watendaji wa mamlaka ya kuzuia rushwa lawamani

Thu, 14 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar.  Asasi za kiraia kisiwani Zanzibar zimelitaka Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi dhidi ya maofisa wake wanaodaiwa kuvamia ofisi za za mamlaka ya kuzuia rushwa na uhujumu wa uchumi Zanzibar (ZAECA) na kuwapiga watendaji wa mamlaka hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Februari 13, 2019 na mkurugenzi wa chama cha wanasheria wanawake Zanzibar, Jamila Mahmoud katika mkutano na waandishi wa habari.

Amesema  kitendo cha maofisa hao hakipaswi kufumbiwa macho, kwamba miongoni mwa waliokumbana na vipigo ni mjamzito.

Amebainisha kuwa polisi kuvamia ofisi za Serikali ni kinyume na sheria na utawala bora na hakipaswi kufumbiwa macho.

“Hakuna mtu alie juu ya sheria ikiwa kuna mtu amefanya kosa lazima awajibishwe kwa mujibu wa sheria,” amesema.

Meneja wa utetezi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa) visiwani Zanzibar, Hawra Shamte amesema lazima kila mtu awajibike ipasavyo.

Amesema haiwezekani maofisa wa polisi kuvamia ofisi zinazojihusisha na mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa na kuwapiga.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz