Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maofisa polisi wanaodaiwa kuua wafikishwa kortini

Napeepic Data Maofisa polisi wanaodaiwa kuua wafikishwa kortini

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa saba wa Jeshi la Polisi mkoani Mtwara ambao wanatuhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Musa Hamis (25) wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mtwara kwa ajili ya kesi yao kutajwa.

Washtakiwa hao wamefikishwa leo Jumanne Februari 8, 2022 wakiwa chini ya ulinzi mkali.

Washtakiwa wanaohusishwa na mauaji hayo ni ofisa Upelelezi (OC CID) Wilaya ya Mtwara, Gilbert Kalanje Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara (OCS), Charles Onyango, Ofisa wa Intelijensia ya Jinai Mkoa wa Mtwara, Charles Kisinza na Mkaguzi wa Polisi, John Msuya pamoja na Mganga Mkuu wa Zahanati ya Polisi, Marco Mbuta. Wengine ni Mkaguzi wa Polisi, Shirazi Mkupa na Koplo Salimu Juma Mbalu.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 25 na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia.

Siku hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Lugano Kasebele ilidaiwa kuwa Januari 5, maofisa hao wa polisi walimuua Musa Hamis Hamis (25), mkazi wa Nachingwea mkoani Mtwara.

Kesi bado haijaanza hata hivyo waandishi wa habari wamezuiwa kuingia chumba cha mahakama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live