Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maofisa 7 wa Polisi wanaodaiwa kuua wapandishwa tena kizimbani

Watuhumiwa Mtwara (600 X 590) Maofisa 7 wa Polisi wanaodaiwa kuua wafikishwa tena mahakamani Mtwara

Tue, 22 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa saba wa Polisi mkoani Mtwara wanaotuhumiwa kufanya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Mussa Hamis (25) wamewasili katika mahakama ya wilaya ya mkoani hapa kwa ajili ya kesi yao kutajwa leo Jumanne Februari 22, 2022.

Washtakiwa hao ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi cha Mtwara, Charles Onyango, Mrakibu wa polisi aliyekua Mkuu wa Intelijensia, Nicholaus Kisinza, Mkaguzi wa Polisi, John Msuya na Mkaguzi Msaidizi wa polisi.

Wengine ni pamoja na Marco Mbuta, Mkaguzi wa Polisi Shirazi Ally Mkupa,  Mrakibu wa Polisi aliyekua Mkuu wa Upelelezi, Gilbert Kalanje,  askari namba G5158 Kopro Salum Juma Mbalu.

Watuhumiwa hao wamefika mahakamani hapa saa 2:57 asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 25 na kusomewa shitaka la mauaji ya kukusudia. Kesi hiyo ilitajwa tena Februari 8, ambapo maofisa hao walifikishwa mahakakani hapo.

Tofauti na awali leo waandishi wameruhusiwa kuingia chumba cha mahakama kupiga picha kabla kesi haijaanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live