Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka yafafanua madai ya mwili wa mfanyabiashara kuwa na dawa za kulevya

32868 Pic+dawa Tanzania Web Photo

Sat, 22 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imesema uchunguzi uliofanyika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili umebaini kuwa mwili wa mfanyabiashara Happy Mboya (38), aliyefariki dunia katika Hospitali ya Mwananyamala haukuwa na dawa za kulevya.

Happy alifariki dunia Desemba 16 na mwili wake ulipangwa kusafirishwa juzi kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi, lakini polisi Kituo cha Oysterbay waliuchukua na kuupeleka Muhimbili kufanyiwa uchunguzi.

Akizungumza na Mwananchi juzi usiku, Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Rogers Siyanga alisema baada ya kufanyiwa uchunguzi mwili huo hawakubaini kuwa na dawa za kulevya kama ilivyoelezwa.

“Maofisa wetu wa DCEA walikuwepo wakati mwili wa marehemu Happy unafanyiwa upasuaji. Haujakutwa na dawa za kulevya kama ilivyodaiwa,” alisema Siyanga.

Baba mdogo wa marehemu, Ally Bilali juzi alilieleza Mwananchi kuwa baada ya kurejea nchini, Happy alifikia katika nyumba ya kulala wageni ambayo haikufahamika na mtu mwingine isipokuwa mume wake. “Hata dada yake alikuwa hafahamu kuwa amesharudi kwa sababu alidai kuwa simu yake imeharibika na wasingeweza kuwasiliana kumbe ilikuwa kumficha. Alipata taarifa baada ya mdogo wake kuzidiwa na wahudumu kumpigia simu ndipo alienda kumchukua kumuwahisha hospitalini,” alisema.

Bilali alisema baada ya kufika hospitalini na kupimwa Happy alionekana kuwa na njaa kali jambo ambalo lilimlazimu daktari kumuandikia dripu za maji ili kumsaidia.

“Lakini hizo dripu hakuwekewa na hatukuambiwa sababu ya msingi hadi alipofariki.”

Mwili wa Happy uliagwa jana mchana Muhimbili.



Chanzo: mwananchi.co.tz