Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamlaka ni ya Jaji Mkuu kesi za ubakaji

44556 Pic+jaji Mamlaka ni ya Jaji Mkuu kesi za ubakaji

Mon, 4 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Unguja. Kutokana na marekebisho ya sheria ya udhalilishaji wanawake na watoto ikiwamo ubakaji, wananchi wametakiwa kufahamu kuwa Jaji Mkuu ndiye mwenye mamlaka pekee kutoa dhamana kwa kesi za aina hiyo pamoja na makosa mengine ya jinai.

Ufafanuzi huo ulitolewa na mwanasheria kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali Salim Mohammed Abdallah, alipotoa elimu ya makosa ya jinai yanayohusu udhalilishaji katika jimbo la Pangawe mkoa wa Mjini Magharibi.

Abdallah alisema kwa mujibu sheria ya udhalilishaji, jaji mkuu ndiye mwenye mamlaka ya kutoa dhamana kwa mshtakiwa.

Katika hatua nyingine, ofisa huyo alisema jamii inapaswa kutambua kuwa mahakama za wilaya na mikoa hazina uwezo wa kisheria kutoa dhamana kwa washtakiwa wa makosa hayo.

Hata hivyo, Abdallah alisema lazima watu watambue matukio ya udhalilishaji wanawake na watoto ni yanaichafua jamii.

Naye mwakilishi wa Pangawe Khamis Juma Maalim, alisema elimu kuhusu kesi za udhalilishaji inahitajika ili jamii ipate kuwa na mwamko.

Maalim alisema mkakati wa viongozi wa kuwaelimisha wananchi kuhusu sheria hizo utasaidia kupunguza matukio hayo.

Mwakilishi huyo alisema zoezi la utoaji elimu litakuwa endelevu katika shehia nyingine ili wananchi wapate mwamko na kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekiathiri.

Awali, mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar Jamila Mahmoud, alisema kuna tatizo kubwa la uelewa wa masuala ya kisheria hususan zinazohusu makosa ya udhalilishaji.

Jamila alieleza kuwa anaamini mikakati zaidi ya kutoa elimu kuhusu udhalilishaji na madhara yake katika jamii inahitajika ili Zanzibar iendelee kubaki salama.



Chanzo: mwananchi.co.tz