Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia washiriki mazishi ya msichana aliyeuliwa na mzazi mwenzie

Sat, 29 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Songea. Simanzi imegubikwa wakati wa mazishi ya Veronica Kayombo (29) anayedaiwa kuuawa na mzazi mwenzake ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Batisin Sanga.

Veronica ambaye ni mkazi wa Msamala kwa Gasa, Songea mkoani Ruvuma anadaiwa kuuawa na mpenzi wake huyo juzi Alhamisi Desemba 27 katika kambi ya JWTZ Chandarua Songea alipokwenda kudai mtoto wake, Grace Sanga (5).

Mamia ya watu wamejitokeza katika mazishi ya Veronica yaliyofanyika leo Jumamosi Desemba 29, 2018 kwenye makaburi ya Msamala Kwa Gasa na kuhudhuriwa na wabunge, madiwani, viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa.

Akiongoza misa ya Mazishi, Paroko wa Magagura, David Mhagama amelaani tukio hilo akisema ni ukatili mkubwa uliofanyika na marehemu amekufa kishujaa kwa kwenda kudai mwanae aliyechukuliwa na kutoroshewa Tanga kwao na mtuhumiwa.

Baba wa marehemu, Hironimus Kayombo anasema ameumia kumpoteza mwanaye wa kwanza Veronica ambaye alikua faraja na kila kitu na ambaye pia alikua rafiki na tegemeo lakini hana cha kufanya zaidi anamwachia Mungu.

Amesema, pigo hilo ni kubwa kwake na familia nzima hata hivyo ameiomba mahakama iache kumtuma mtu akiwa na ugomvi na mwenzie kupeleka fomu kwa mgomvi mwenzie.

"Nina amini iwapo mwanangu asingepewa hizo fomu kumsainisha mzazi mwenzie pengine mwanangu angekua hai hadi muda huu, namuachia Mungu kwani siwezi kufanya chochote leo nina maumivu makubwa," amesema Kayombo.

Amesema siku ya tukio hilo, mwanae aliamka mzima na nilimpeleka mimi mwenyewe mahakamani na kumuacha akifuatilia masuala ya mwanae kwani alikua akiomba apewe mwanae.

Shuhuda wa tukio hilo Jamila Said ambaye ni rafiki wa marehemu Veronica amesema hatakaa asahau tukio hilo kwani ukatili huo ni wa kutisha na pigo aliloachiwa ni kubwa kwa kuwa marehemu alikua mtu muhimu kwake.

Amesema ameshuhudia rafiki yake akipigwa risasi, rafi

Chanzo: mwananchi.co.tz