Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mamia wafurika mahakamani rufaa ya dhamana ya Mbowe

29241 Pic+mbowe TanzaniaWeb

Thu, 29 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Viongozi, wanachama na wafuasi wa Chadema na vyama rafiki wamefurika katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kusikiliza rufaa ya dhamana ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema), Ester Matiko.

Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na Matiko ambaye pia mweka hazina wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) wamekata rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo baada ya kupatikana na kosa la kukiuka masharti ya dhamana waliyopewa awali.

Walifutiwa dhamana hiyo Novemba 23 na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kufuatia maombi ya upande wa mashtaka kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana kwa kutokufika mahakamani tarehe ambazo kesi yao ilipangwa kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.

Rufaa yao imepangwa kusikilizwa leo na Jaji Sam Rumanyika.

Mbowe na Matiko ambao wako mahabusu katika Gereza la Segerea walifikishwa mahakamani hapa mapema leo asubuhi na sasa rufaa yao inatarajiwa kuanza kusikilizwa mahakamani hapo muda wowote.

Miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliofika mahakamani hapo ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, John Mnyika, wabunge na madiwani.

Endelea kufuatilia Mwananchi

 



Chanzo: mwananchi.co.tz