Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo ya Ndani yaagiza kufuata sheria na miongozo

Kady Chis Kadio

Sat, 12 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio ambaye pia ni Mlezi wa Mfuko wa Faraja ameagiza uongozi wa mfuko wa faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuzingatia katiba na mwongozi wa mfuko huo kwenye ukusanyaji wa mapato, matumizi ya fedha za mfuko huo na huduma kwa wanachama wake.

Akizungumza na uongozi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi amewaelekeza kuingiza mchango wa mwajiri kwenye bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2022/23 ili kuhudumua wanachama wa mfuko huo. Pia amewaagiza kufanya uchaguzi wa Uongozi wa kudumu wa mfuko ndani ya mwaka huu wa fedha.

“Mimi kama Mlezi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi nawasisitiza kuzingatia katiba na mwongozo wa Mfuko hii pamoja na kuingiza mchango wa nwajiri kwenye bajeti ya Wizara” amesema

Christopher Kadio amesema hayo kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi uliofanyika katika ukumbu wa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto, jijini Dodoma.

Aidha amewashauri watendaji na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kujiunga na Mfuko huo kwani faida zake ni nyingi na utawawezesha wafanyakazi kiuchumi na kuongeza tija kwenye majukumu yao.

Katibu Mkuu Christopher Kadio amesema kwamba Mfuko wa Faraja wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni kama sehemu ya bima ya dharura na kwamba utasaidia kupunguza msongo wa mawazo wa changamoto za masuala ya dharura ya kijamii kama kuuguliwa na kufiwa.

“Licha ya kwamba kujiunga na Mfuko ni hairi ya mtu,lakini kwa faida nilizozieleza ni ushauri wangu kuwa watu wote wajiunge kwa kuzingatia faida nilizozieleza, Umojani nguvu na utengano ni udhaifu” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live