Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama wa mwanakwaya aliyefariki gesti asimulia alivyopokea ujumbe wa muuaji

16172 Pic+gest TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

 Mama mzazi wa mwimbaji wa Kwaya ya Vijana ya Kanisa la AICT Chang'ombe (CVC), Mariam Charles (22), Ester Charles amesimulia kwa uchungu namna alivyopata taarifa za binti yake kuuawa siku chache kabla ya kulipiwa mahari.

Mwili wa Mariam ulikutwa katika nyumba ya kulala wageni ya 'East London’ iliyopo Buza anakodaiwa alikuwa na mchumba wake.

Akizungumza na MCL Digital leo Septemba 7, mama huyo amesema Septemba 4 mwanae alimuaga kuwa anaenda kanisani kwenye kwaya.

“Baadaye akaniambia ameitwa na mchumba wake hivyo anaenda kuonana naye. Sikuwa na wasiwasi kwa sababu ni mchumba wake na binti alikuwa akiaga popote anapoenda," amesema.

Amesema baadaye alishangaa kupata ujumbe kutoka kwa mchumba wa mtoto wake unaosema; “Tayari nimemuua mwanao.”

"Nilishtuka na ikabidi tuanze kumtafuta Mariam na tukaenda polisi. Kusema kweli tangu hapo hali yangu nikawa sielewi hadi tulipokuja kuona kweli amemuua," amesema na kuongeza;

 

"Binti yangu alikuwa mpole, mnyenyekevu, hana ugomvi na mtu na aliniaga kila anakoenda.”

Dada wa Mariam, Pendo Lutonya amesema amesikitishwa na kifo cha kinyama cha mdogo wake kwa sababu badala ya kupokea mahari kama ilivyodaiwa, ameuawa.

"Mara ya mwisho nilikutana naye kanisani wiki iliyopita na alikuwa anaenda Morogoro kwenye huduma, sijamuona tena hadi leo mdogo wangu ameuawa," amesema.

Soma zaidi: Mwili wa mwanakwaya wa kanisa la AICT wakutwa gesti, mchumba wake ahusishwa

Chanzo: mwananchi.co.tz