Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama na watoto watano wanusurika kuuawa Kiteto

Mama Kanusurika Mama na watoto watano wanusurika kuuawa Kiteto

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mariamu Ramadhani na watoto wake watano wakazi wa wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, wamenusurika kuuawa na mtalaka wake walioachana miaka 17 iliyopita

Submitted by exaud on Jumanne , 23rd Aug , 2022Inaelezwa kuwa mwanaume huyo alifika nyumbani kwa mwanamke huyo akiwa na Panga, Kisu na Sururu ambapo mwanamke aliamua kukimbia kabla ya mwanaume huyo kuanza kubomoa nyumba na kuiba baadhi ya mali

Baadhi ya mashuhuda wameliomba Jeshi la Polisi Kiteto kufuatilia tukio hilo ili liwe fundisho pamoja na kwamba vitendo vya ukatili Kiteto vimetajwa kukithiri.

Hata hivyo baada ya mtalaka huyo kutoweka katika mazingira hayo mwanaume huyo aliishia kubomoa nyumba kisha kuingia ndani na kuchukua fedha taslimu shilingi laki mbili za mtalaka na kutoweka kusikojulikana.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live