Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama na bintiye watuhumiwa kuua kisa Sh150,000

Mauajipicc Data Mama na bintiye watuhumiwa kuua kisa Sh150,000

Fri, 18 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoani Manyara linawashikilia mama na mtoto wake kwa tuhuma za kumuua muuza mkaa kwa madai ya kuwadhulumu Sh150, 000

Akizungumza leo Ijumaa Machi 18, 2022 Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Benjamin Kuzaga amesema tukio hilo limetokea Machi 12 katika  kijiji cha Langai ambapo mama na mtoto wanatuhumiwa kumuua mfanyabishara huyo Robert John (51) kwa kumchoma kisu na kumkata panga.

Kamanda Kuzaga amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Aisha Shabani (40) mkazi wa Rombo mkoani Kilimanjaro na mama yake Amina Shabani (70) mkazi wa Busi wilayani Kondoa.

"Chanzo cha kifo hicho ni ugomvi wa mama na Robert. Mama alikuwa anamdai Robert Sh150,000 alizopewa kwa ajili ya kuwaletea mkaa," amesema kamanda Kuzaga.

Amesema wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashataka yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live