Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama muuza mboga apigwa na mgambo hadi kulazwa

Mama Muuza Mboga Apigwa Na Mgambo Hadi Kulazwa Mama muuza mboga apigwa na mgambo hadi kulazwa

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: Wasafi TV

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Aziza Juma mkazi wa Manispaa ya Morogoro anaye jishugulisha na biashara ya kuuza mboga mboga amepigwa na kujeruhiwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni mgambo wa Manispaa hiyo wakimtuhumu kufanya biashara katika maeneo yasiyoruhusiwa.

Mama huyo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro akiendelea kupatiwa matibabu kutokana na tukio hilo amesema mgambo hao walimkamata na kuanza kumpiga kwa kutumia magongo na kumwagiwa maji.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Abdulaziz Abood amefika wodini na kumjulia hali mama huyo na kuahidi kuchukua hatua dhidi ya wahusika wa tukio hilo.

Chanzo: Wasafi TV