Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama mbaroni kwa kunyonga, kujeruhi wanae

Kunyonga Mama Mama mbaroni kwa kunyonga, kujeruhi wanae

Tue, 29 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja aitwae Paschalina Geay (59) mkazi wa mtaa wa Angoni "A" wilaya ya Babati mkoa wa Manyara anashikiliwa na Polisi Manyara kwa kosa la kumuua Mtoto wake wa kiume Nada Peter (6) kwa kumnyonga shingo na Kisha kumjeruhi katika paji la uso kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

RPC Manyara, Limited Mhongole amesema tukio hilo limetokea tarehe 26/03/2022 ambapo baada ya Mtuhumiwa kutekeleza mauaji hayo alimshambulia Mtoto wake mwingine Dawii Peter (4)kwa kumpiga maeneo mbalimbali ya mwili wake na kumvunja mkono wa kulia na lengo ikiwa ni kumuua pia Mtoto huyo.

Kamanda Mhongole amesema uchunguzi wa awali umeonesha Mtuhumiwa huyo ana matatizo ya afya ya akili na hivyo upelekezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live