Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama mbaroni kwa kumuua mtoto wake kwa fimbo

11921 Pic+mama TanzaniaWeb

Tue, 14 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wanawake wawili wanashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma mbalimbali akiwamo mmoja aliyemuua mtoto wake wa kiume wa miaka 11 kwa kumpiga fimbo kichwani.

Katika tukio jingine mwanamke mwingine anashikiliwa na polisi akituhumiwa kumsokomeza mwiko sehemu za siri mtoto wa dada yake mwenye umri wa miaka sita.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema hayo leo Agosti 14 wakati akitoa taarifa ya matukio mbalimbali ya mkoani humo kwa waandishi wa habari.

Kamanda Mutafungwa amesema matukio yote yametokea katika wilaya za Gairo na Manispaa ya Morogoro na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani mara moja.

Chanzo: mwananchi.co.tz