Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama atupwa jela maisha kwa kumbaka mvulana wa miaka 15

RAPE Mama atupwa jela maisha kwa kumbaka mvulana wa miaka 15

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Mtwara imemhukumu kifungo cha maisha jela, Asha Ismail Chanchoni (47) kwa kosa la shambulio la aibu, baada kujihusisha kimapenzi na mvulana mwenye umri wa miaka 15.

Hukumu hiyo imetolewa Aprili 2, 2024 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Lucas Jang'andu aliyesema Mahakama imethibitisha bila kuacha shaka kuwa mwanamke huyo alikuwa akijihusisha kimapenzi na mvulana huyo.

Kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani na mashahidi wawili wa upande wa Jamhuri, tukio hilo lilitokea Februari 2023 katika mtaa wa Chuno katika manispaa ya Mtwara Mikindani anakoishi mwanamke huyo.

Akichambua ushahidi, Hakimu Jang'wandu alisema siku ya tukio mshtakiwa alimbaka mtoto huyo kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kutoka kwa mashahidi mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live