Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama amuua mwanaye wa kambo, ajisalimisha polisi

Mama Amuua Mwanaye Wa Kambo, Ajisalimisha Polisi Mama amuua mwanaye wa kambo, ajisalimisha polisi

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: Radio Jambo

Polisi katika kaunti ya Kisii wanamzuilia mwanaume mmoja kutoka eneo la Bonchari baada ya kukiri kumuua mwanawe wa kambo.

Sebastian Matundura, 61, alijisalimisha katika kituo cha polisi siku ya Jumatatu ambapo alikiri kutekeleza mauaji hayo Jumapili usiku.

Mkuu wa polisi wa Gesonso Charles Machinji amesema mshukiwa alikiri kwamba alimgonga mwanawe kichwani kutumia jembe wakati walipokuwa wakipigana nyumbani kwao Igonga kufuatia mzozo wa kinyumbani.

Baada ya kumgonga kwenye kichwa, mshukiwa alimdunga mwanawe huyo wa kambo kwa kutumia kisu kabla ya kutoweka.

Anadaiwa kutafuta maficho katika nyumba ya majirani zake kabla ya kujisalimisha kwa polisi siku ya Jumatatu.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika mochari huku uchunguzi wa polisi ukiendelea.

Haya yanajiri siku mbili tu baada ya polisi kumtia mbaroni mwanaume mmoja katika eneo la Nyamache, kaunti hiyo ya Kisii kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya watoto wake wawili siku ya Ijumaa asubuhi.

Mwanamume ambaye kwa sasa yuko kizuizini anadaiwa kuwakata vichwa watoto wake wawili na kutupa miili yao kwenye shamba la familia katika kijiji cha Kiobegi. Polisi walimkamata muda mfupi baadaye.

Majirani walisema mwanamume huyo amekuwa na shida ya akili kwa miaka kadhaa.

Chanzo: Radio Jambo