Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama amchoma moto mwanaye kisa ameiba 'jero'

Bibi Awachoma Moto Mama amchoma moto mwanaye kisa ameiba 'jero'

Sun, 7 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto mwenye umri wa miaka 10 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Lutozo amejeruhiwa kwa kuunguzwa na kisu chenye moto maeneo mbalimbali ya mwili wake na mama yake wa kambo ajulikanaye kwa jina la Jawila Ghalib mwenye umri wa miaka 28 kwa madai ya mtoto huyo kaiba shilingi 500.

Akizungumza nasi mtoto huyo pamoja na kaka yake wamesema baada ya mama yao wa kambo kuwauliza nani alichukua hela yake shilingi mia tano ndipo mtoto huyo alikiri ni yeye ameichukua na kununua mandazi ndipo alipochukua maamuzi ya kumjeruhi mtoto huyo sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia kisu cha moto.

“Niliiba ndani mia tano ndo mama akanichoma alikuwa anaweka kisu kwenye moto arafu ananiunguza alikuwa amenifunga mikono na miguu baadae alipomaliza akanifungulia ” alisema mtoto huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live