Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama aliyetrend akimfanyia unyama mwanaye, kupimwa akili

Dorothy Nabulime.png Dorothy Nabulime

Tue, 6 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi huko Uganda leo litamfikisha Mahakamani Mama mmoja aitwaye Dorothy Nabulime (22) mkazi wa mji mdogo wa Busula, nje kidogo ya jiji la Kampala ambaye video zilizosambaa mtandaoni anaonekana akimchapa bila huruma mtoto wake mdogo wa miaka miwili.

Kabla ya kumfikisha kesho Mahakamani, Polisi wanasema wamempeleka kumpima akili mama huyo aliyezua gumzo kubwa na kujiridhisha mama huyo yuko sawa kiakili hivyo watamfikisha Mahakamani kesho kwa unyanyasaji huo wa mwanae.

Tayari mtoto wake amechukuliwa na kituo cha kulelea watoto na sasa Polisi wanamtafuta Baba wa mtoto huyo ambaye wamekuwa na mgogoro na mama huyo.

Dorothy mama wa watoto watatu alirekodiwa video akimpiga mwanae huyo bila huruma na kumuangusha kwenye beseni alilokua anaogea.

Mwanae mkubwa ana miaka 5 ambaye alimzaa akiwa na miaka 17. Wa pili ana umri wa mitatu na wa mwisho ana miaka miwili ambaye ndiye aliyerekodiwa akimpiga.

Dorothy ni “single mother” ambaye anadaiwa kupitia unyanyasaji wa kijinsia katika malezi yake, na anawalea watoto wote watatu peke yake kwa biashara ndogondogo.

Amefunguliwa kesi ya shambulio la kudhuru mwili (assault causing bodily harm) na unyanyasaji wa mtoto (child abuse) na anatarajiwa kupandishwa kizimbani kesho, jumatatu kujibu tuhuma zinazomkabili. Kwa sasa anashikiliwa kituo cha polisi Luwero, huko Busula na amefunguliwa kesi nambari SD/RF/06/03/09/2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live