Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama adaiwa kuwatelekeza watoto wake, polisi wamsaka

Mama Adaiwa Kuwatelekeza Watoto Wake, Polisi Wamsaka Mama adaiwa kuwatelekeza watoto wake, polisi wamsaka

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamtafuta Mariamu Salumu mkazi wa Kisesa mkoani Mwanza kwa tuhuma ya kutelekeza watoto wake wawili wenye umri chini ya miaka 18 na kusababisha kuishi katika mazingira hatarishi huku likimshikilia James Julius mkazi wa Kahama kwa kuishi na watoto hao kinyume cha sheria.

Aidha ndugu wa James wanatoa rai kwa mama kujitokeza kwani watoto wake wanaishi kwa shida hasa huyo mdogo kwani kwa umri alionao anamuhitaji zaidi mama yake kuliko mtu yeyote.

Ndugu wa James wanaendelea kumtaka mama huyo ajitokeze kwani anamuweka ndugu yao James matatani kwani hadi sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live