Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama adaiwa kumuua mwanaye wa kumzaa kwa kumchinja

FB IMG 1670076258758 Saada Mama adaiwa kumuua mwanaye wa kumzaa kwa kumchinja

Sat, 3 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unyama wa kutisha! Tukio la kinyama limetokea jijini Dar es Salaam baada ya mama mmoja mkazi wa Mbezi Magari Saba kuaiwa kumuua mwanaye wa kumzaa aitwaye Saada (pichani) kwa kumchinja shingoni na kumponda na kitu kizito huku chanzo kikidaiwa kuwa ni imani za kishirikina.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni nyumbani kwao na marehemu ambapo mama baada ya tukio hilo, meno na ulimi wa marehemu vilikutwa vimesambaa sebuleni kwenye eneo hilo la tukio huku ikidaiwa kuwa mama huyo alifanya mauaji hayo akishirikiana na watoto wake wengine.

Wakizungumzia tukio hilo, mashuhuda wamesema kuwa siku ya tukio, mama Saada alimwambia mpangaji wake kuwa ikifika saa 12 jioni hakuna kutoka kwenye chumba chake, hivyo kama kupika na vitu vingine vikamilike kabla ya muda huo kwa kuwa kutakuwa na kazi wanafanya usiku.

Mama Saada alimuomba mpangaji huyo kuwa iwapo yuko tayari aungane naye kumsaidia, lakini mpangaji alikataa na hata ilipofika usiku jirani huyo alisikia makelele ya marehemu Saada akilia "msiniue mimi sio jini mama ni mwanao mama, nakupenda mama".

Hata hivyo chanzo kinazidi kueleza kuwa wakati mama huyo akitekeleza mauaji hayo na wanaye wengine, walisikika wakisema "ua jini huyo..."

Watuhumiwa hao walidhani kuwa wanaomuua ni jini anayemsumbua mtoto wake, ambaye wiki chache alikuwa akipandisha mashetani, na katika dua hiyo ya mauaji ikiongozwa na ustadhi aliyekuwa akisoma dua hiyo, ambaye inasemekana kuwa ni mjomba pia wa marehemu.

Watuhumiwa wa tukio hilo ambao ni Mama Saada na wanaye wengine wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live