Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malumbano shahidi kukutwa na diary kesi ya kina Mbowe

Mbowe Kesipic Malumbano shahidi kukutwa na diary kesi ya kina Mbowe

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Malumbano ya kisheria yameibuka mahakamani leo katika kesi ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu kuhusiana na uhalali wa shahidi kupanda kizimbani akiwa na shajara (diary) katarasi, simu na kalamu ambavyo vinadaiwa na upande wa utetezi kuwa shahidi huyo alikuwa akivitumia wakati akitoa ushahidi wake Ijumaa iliyopita.

Kutokana na madai hayo mawakili hao wa utetezi wameiomba mahakama iamuru kuwa shahidi huyo amekiuka kiapo chake cha kutoa ushahidi wa kweli na iamuru ushahidi wake alioutoa uondolewe kwenye kumbukumbu za mahakama.

Hata hivyo upande wa mashtaka umepinga hoja na madai hayo ya upande wa utetezi, jambo ambalo liliibua mvutano wa hoja za kisheria baina ya pande hizo mbili.

Mvutano huo wa hoja za kisheria umeibuka muda mfupi baada ya mahakama kutoa uamuzi wa pingamizi lililoibuliwa na mawakili wa utetezi Ijumaa wakipinga barua ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, ambayo shahidi huyo aliiomba mahakama iipokee kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa mashtaka.

Barua hiyo ndiyo inayompa mamlaka shahidi huyo ya kuwasilisha mahakamani hapo Kitabu cha Kumbukumbu za Mahabusu (DR) katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam cha mwaka 2020, kwa lengo la kuthibitisha kuwa mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo Adamu Hassan Kasekwa na wa tatu Mohamed Abdillahi Ling’wenya walihifadhiwa kituoni hapo.

Katika uamuzi wake, Jaji Joachim Tiganga ametupilia mbali hoja za pingamizi la mawakili wa utetezi na akaamuru barua hiyo ipokewe kama kielelezo cha upande wa mashtaka, na baada ya uamuzi huo, ndipo mawakili hao wa utetezi wakaibua hoja ya shahidi kukutwa na vitu hivyo kizimbani.

Hapa ni mwanzo mwisho malumbano ya mawakili;

Wakili wa utetezi Mtobesya: Pamoja na mahakama kupokea kielelezo, Ijumaa kuna hoja iliibuka na sisi tunapinga shahidi kuendelea kutoa ushahidi hadi itakapoamuliwa.

Shauri hili ni shauri la uhujumu uchumi, Ijumaa upande wa utetezi kupitia Peter Kibatala walitoa hoja wakati mahakama inaendelea ilionekana shahidi namba mbili alikuwa na diary, kalamu na simu wakati Kibatala anatoa hiyo hoja diary ilikuwa wazi.

Mahakama ilielekeza vitu hivyo kuletwa mbele ya mahakama lakini baadae ikaelekeza kurudishiwa simu na kalamu.

Mahakama ilielekeza pande zote mbili kukaa na kuona namna kushughulikua suala hili

Leo tutaeleza kwanini hatupo tayari kuendelea na huyu Shahidi.

Leo tunaomba mahakama kutumia power yake ya asili ingawa hakuna kifungu kilichoelekeza mahakama kutumia power yake ya asili

Ukisoma kifungu cha 28 Sura 200 ya mwenendo wa makosa ya jinai kama kilivyofanyiwa marekebisho 2019 kifungu cha 264 kinaelezea power ya mahakama kuu.

Wakili Mtobesya: Tunaomba mahakama ichukulie kitendo cha Shahidi kuwa na diary wazi wakati mahakama inaendelea ni kitendo cha reliable and competent.

Suala la kutoa ushahidi linaongozwa na sheria za ushahidi

Ukisoma sheria za ushahidi pamoja na general police order mtu ambaye ni askari wakati wa kutoa ushahidi hatakiwi kuwa na material yoyote hadi pale ruhusa ya mahakama.

Wakili Mtobesya: Ruhusa hiyo ataipata pale ambapo atahitaji kureflesh memory na sio sehemu nyingine yoyote ile na haya tunayasema chini ya kifungu cha 168 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya ushahidi na PGO 282 aya ya 7

Wakili Mtobesya: Kwa nini kuna utaratibu wa kufuata ni ili mshtakiwa aweze kupata haki yake hasa wakati wa kuuliza maswali kwa mujibu wa kifungu cha 172 cha sheria ya ushahidi.

Ikitokea shahidi anafanya hivyo kwa kificho inamnyima mtuhumiwa haki yake

Wakili Mtobesya: Unapokuta diary iko wazi huwezi kujua kulikuwa na nini wakati mwingine alikuwa anajikumbusha na alikuwa nayo kizimbani tangu ameingia.

Maombi yetu Mheshimiwa Jaji Shahidi huyu hatakiwi kuwa relay able na kwa kuwa ameifanya akiwa hajamaaliza kutoa ushahidi.

Wakili Mtobesya: Sababu zilizoelezwa katika kifungu cha 127 cha sheria za ushahid ni nyingi sisi ni submission yetu kuanzia pale alipoishia Ijumaaa asiendelee na ushahidi alioutoa na mahakama iuondoe kwenye kumbukumbu zake na yeye pia kuondolewa.

Wakili Mtobesya: Hata sasa ushahidi uliingia wa kielelezo cha barua uondolewe kwa kuwa umetokana na shahidi huyu.

Shahidi na ushahidi alioutoa uondoke kwenye kumbukumbu za mahakama na yeye pia aondolewe ni hayo tu Mheshimiwa.

Wakili Peter Kibatala: Tangu shahidi kuapishwa hii ndio msingi

kizimba hakitakiwi kuwa na kitu kingine chochote zaidi ya vifaa vya uwapishwaji vitu vingine vitakavyoingizwa lazima kipate kibali cha mahakama.

Shahidi hatakiwi kushika kitu kingine hadi pale mahakama itakapomuaga kumruhusu kuondoka.

Tunaialika mahakama na wakati wa kuandaa uwamuzi kuangalia kwenye chumba cha mtihani mtu anapokutwa na material mengine yoyote nini kinachofanyika anakuwa disqualification.

Wakili Peter Kibatala: Hiyo diary aliyokutwa nayo imetoka mahakamani na kuingia mahakamani ikiwa kwenye mikono ya shahidi

Muda tuliosimama kutoa hoja kulikuwa na zoezi lingine la kisheria.

Wakili Mtobesya alirejea kwenye kifungu cha 127 cha sheria ya ushahidi ambapo kuna maneno ambayo hayajaandikwa moja kwa moja lakini inaipa mahakama nguvu.

Kifungu cha 62 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya ushahidi kina taka shahidi kutoa ushahidi wake mwenye kutoka ndani ushahidi wa oral.

Shahidi aliyekuwa na material bila kuomba ruhusa alikuwa anatoa ushahidi usiokuwa original wala haukuwa wake hivyo hana sifa.

Shahidi anayeingia na material yasiyofahamika ni shahidi asiyejua jukumu lake

Tunafahamu itakuwa hoja shahidi akiwa ni afisa wa Polisi anatakiwa kuwa na note book lakini kuna limitation

Wakili Kibatala: Kuna vifungu katika PGO 282(5) na 286 kuna masharti yaliyowekwa hata hiyo not book inatakaiwa kuandikwa kwa penseli

PGO ya 8C inasema kama Shahidi angesema ana not book.

Tuna malizia kwa hoja hii kuwa shahidi huyu hana sifa na tunaomba aondolewe

Utakumbuka siku niliposimama na kusema shahidi huyu hana sifa

Tunaomba diary ikaguliwe kama kuna majina ya maaskari wenzake alipokuwa anawataja isiishie hapa ifungwe na airudishiwe ikaguliwe na mahakama ichukue hatua

Wakili wa Serikali Mwandamizi Abdallah Chavula anasima kwa ajili ya kujibu hoja za utetezi.

Ni msimamo wetu kwamba hatukubaliani na msingi wa hoja za wenzetu lakini pili hatukubaliani na maombi yaliyotolewa na wenzetu

Wakili Chavula: Wenzetu wamedai kwamba shahidi akiwa kwenye kizimba na diary, kalamu na simu kwa mujibu wao vitu hivyo alivyoonekana navyo havitakiwi kuwa navyo kwenye sehemu ya kutolea ushahidi na kuielekeza mahakama kwenye kifungu cha 168 Sura 6 kama kilivyofanyiwa marejeo 2019 na PGO 282 kifungu kidogo cha 7.

Vifungu hivi kwa ujumla wake vinatoa katazo kwa shahidi Kutoingia na kitu chochote kwenye kizimba na kuielekeza mahakama kuwa kuna kanuni ambayo inakataza uwepo wa kitu chochote kile kwenye eneo la ushahidi isipokuwa kile kitakachomuwezesha kutoa kiapo

Ni utaratibu na utamaduni unapoielekeza mahakama kwenye kanuni yoyote ile basi ileze mahakama kanuni hiyo inakubalika kisheria?

Basi walau ieleze mahakama kanuni hii inaelezeka na kukubalika bila kufanya hayo yanabaki maneno yasiyoungwa mkono na mamlaka za kisheria

Muheshimiwa Jaji kifungu cha 168 cha sheria ya ushahidi lugha iliyotumika haina ukakasi ni lugha iliyonyooka ukisoma unapata tafsiri ya moja kwa moja

Haijaeleza ni wapi shahidi akija kutoa ushahidi asiwe na kitu chochote aje na mavazi yake tu kwa heshima zote hatukubaliani nao.

Lingine ni PGO 282(7) na 286 (8) cha kwanza inatoa maelekezo kwa ofisa wa Polisi anapotoa ushahidi wake kuwa na notebook

Sharti la pili kabla ya kwenda mahakamani anatakiwa ajikumbushe kwenye notebook yake

Hiki tunachokiona hapa haitegemewi shahidi ambaye ni askari kutakosekana taarifa ya jambo au ushahidi mahakamani isije kuonekana ni ajabu kwa askari kwenye not book yake kukutwa taarifa ya jambo analoenda kutolea ushahidi.

PGO ya 7b hapa napo ipo wazi kwa ruhusa ya mahakama Jaji au Hakimu mwenye not book kama kuna haja ya kujikumbusha pekee ataruhusiwa kufanya hivyo

Hivi vifungu viwili ukivitaza kwa pamoja havitoi katazo vya yeye Shahidi ambaye na afiasa wa Polisi kuwa na notebook na kama nia ingekuwa ni kuweka katazo ingezungumzwa wazi wazi.

Kanuni ya nane inaongelea suala la inspection na kuna mazingira matatu

Ya kwanza inatoa mamlaka kwa OCS wa wilaya na vituo vya polisi kufanyia uchunguzi na hii ni kuhakikisha zinatunzwa kwa uzuri

Takwa la pili nalo ni la ukaguzi na limeenda mbali zaidi nani anapaswa kuitunza hiyo notebook na ya mwisho ambayo imezungumziwa inatolewa mipaka nani anapaswa kuiona kwa ajili ya kufanyiwa upekuzi.

Watu wengine wenye haki ya kuona notebook ni majaji na mahakimu ambao sheria imewatambua

Notebook hizi zimekuwa na mambo mengine ya siri ndani yanayohusiana na kesi nyingine na ndio maana kukawekwa mipaka ya watu wa kuiona

PGO haijakatazwa shahidi kuwa na not book ilichoelekeza ni wakati wa kufanya rejea

Hoja nyingine ni kuondolewa kwa shahidi na mahakama isizingatie ushahidi wake wakati hayo yanatokea shahidi alikuwa hatoi ushahidi alikuwa akisikiliza malumbano ya hoja na hayo.

Wakati anaongozwa kula kiapo hadi anasimamishwa kusikiliza mapingamizi mahakama ili kuwepo na washtakiwa waliokuwepo kumwangalia shahidi muda wote wakati anaongozwa hakuna aliyesimama kupinga alikuwa anarejea hiyo hoja haikuwepo.

Chanzo: mwananchidigital