Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malkia wa Tembo na wenzake Kusota miaka 15 jela, faini ya mabilioni

A3ba3babbd48a55d6a238c1863b5f35a.png Malkia wa Tembo na wenzake Kusota miaka 15 jela, faini ya mabilioni

Wed, 8 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu kifungo cha miaka 15 jela washitakiwa watatu na kulipa faini ya Sh bilioni 27.8 baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya kuongoza genge la uhalifu na kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 13.9.

Washitakiwa hao ni raia wa China Yang Feng Glan, maarufu ‘Malkia wa Meno ya Tembo’ na Watanzania Salvius Matembo na Philemon Manase.

Hukumu hiyo ilisomwa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaid baada ya kujiridhisha pasipo kuacha shaka yoyote kuhusu mashitaka dhidi ya washitakiwa hao.

Sambamba na hukumu hiyo, aliamuru kutaifishwa mali za Malkia wa Meno ya Tembo ikiwamo shamba lililoko mkoani Tanga.

Kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali, Faraji Nguka aliileza mahakama kuwa shauri hilo lilirejeshwa kwa ajili ya kutekeleza maagizo ya Mahakama Kuu baada ya kutengua hukumu ya awali iliyotolewa Februari 19, 2019 na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hakimu Shaid alisema shauri hilo lilirejeshwa baada ya washitakiwa kukata rufaa Mahakama Kuu ambapo hukumu ya awali ilitenguliwa na kurejeshwa ili hukumu isomwe upya kwa kile alichosema kuwa katika hukumu ya awali hakueleza aliwatia hatia kwa kosa gani.

“Hili jalada hukumu ilitoka, mlipokata rufaa lilirejeshwa kwa ajili ya kusomwa hukumu tena kwa sababu sikueleza nimewatia hatiani kwa makosa gani, mashtaka yalikuwa ni kuongoza genge la uhalifu na kufanya biashara haramu ya meno ya tembo. Mambo niliyozingatia ni kama washtakiwa wanajuana na kama walitenda makosa hayo,” alisema Hakimu Shaid.

Alisema mashahidi katika ushahidi wao walieleza namna mshtakiwa wa kwanza na wa pili walivyofahamiana katika biashara hiyo na kwamba wao ndiyo walikuwa wakusanyaji wa meno ya tembo kupeleka kwa Malkia wa Meno ya Tembo na pia mshtakiwa huyo alivyoyapokea na kuhifadhi nyumbani kwake.

Alisema hakukuwa na shaka yoyote ya washtakiwa hao kujuana kwa kuwa kulikuwa pia na miamala ya simu iliyofanyika kati ya mshtakiwa wa kwanza na wa pili hali iliyothibitisha kuwa wanafahamiana na kuna muunganiko wa mawasiliano baina yao.

Akiomba unafuu wa adhabu kwa niaba ya washtakiwa, Wakili wa Utetezi, Nehemia Nkoko alidai katika uamuzi wa Mahakama Kuu Mheshimiwa Jaji alisema muda waliokaa gerezani washtakiwa hao mahabusu kabla ya hukumu na ule waliotumikia kifungo kabla ya kutenguliwa uzingatiwe katika kutoa hukumu mpya.

“Yeye mheshimiwa Jaji alisema miaka sita lakini sisi hesabu zetu ni miaka 6 tunaomba adhabu ya nafuu hasa ukizingatia mshtakiwa wa tatu ni mama wa miaka 70 na ni mgonjwa, hali ya afyA yake si nzuri,” alisema.

Akisoma huku, Hakimu Shaid alisema kama mwendesha mashtaka alivyosema hana rekodi ya makosa ya awali na wakili wenu amesema mmekaa mahabusi muda mrefu, ni kweli lakini ukweli ni kuwa mliwakosea Watanzania na kukosesha nchi mapato hivyo natoa hukumu kwa kosa la kwanza mshtakiwa wa tatu miaka 15 jela, kosa la pili mashtakiwa wa kwanza na wa pili miaka 15 na kosa la tatu washtakiwa wote watalipa faini mara mbili ya mali waliyokamatwa nayo wakishindwa watatumikia adhabu ya kwenda jela miaka miwili.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live