Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malinzi, Mwesigwa wahukumiwa kifungo miaka miwili jela au kulipa faini

88111 Pic+malinzi+22 Malinzi, Mwesigwa wahukumiwa kifungo miaka miwili jela au kulipa faini

Sat, 14 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatano Desemba 11, 2019 imewahukumu aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na aliyekuwa Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini.

Malinzi ametakiwa kulipa faini ya Sh500,000 na Mwesigwa Sh1 miliomi. Wote wamekubali kulipa kiasi hicho cha fedha. Hata hivyo utaratibu wa kulipa fedha hizo leo umekwama, wawili hao kurudishwa rumande hadi kesho watakapokamilisha taratibu hizo za malipo.

Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo leo Jumatano Desemba 11, 2019 baada ya kuwatia hatiani wawili hao.

Wakati Malinzi akitiwa hatiani kwa shtaka moja la kutengeneza nyaraka za uongo, Mwesigwa alitiwa hatiani kwa kutumia nyaraka hizo.

Mahakama hiyo imewaachia huru washtakiwa wawili katika kesi hiyo ambao ni aliyekuwa mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga na Frola Rauya ambaye alikuwa karani.

Katika shtaka hilo Malinzi anadaiwa kutengeneza nyaraka hizo zinazoeleza kuhusu kikao cha kamati tendaji ya TFF kwa kubadili watia saini badala ya Edagar Masoud aliwekwa Mwanga.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 213/2017 washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 20 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji fedha ambazo ni Dola 173,335 za Marekani.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz