Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makamanda watoa onyo kali wezi wa mafuta SGR

Makamanda Watoa Onyo Kali Wezi Wa Mafuta SGR Makamanda watoa onyo kali wezi wa mafuta SGR

Thu, 12 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza wametoa onyo kali kwa watu wanaohujumu Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Isaka hadi Mwanza kwa kuiba mafuta ya dizeli na vifaa vya ujenzi wakisisitiza kuwa ni lazima mradi huo uwe salama muda wote.

Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mwanza wametoa onyo kali kwa watu wanaohujumu Ujenzi wa Mradi wa Reli ya kisasa (SGR) kipande cha Isaka hadi Mwanza kwa kuiba mafuta ya dizeli na vifaa vya ujenzi wakisisitiza kuwa ni lazima mradi huo uwe salama muda wote. Onyo hilo limetolewa jana Jumatano Januari 11,2023 na Makamanda wa Polisi Mikoa ya Shinyanga (ACP Janeth Magomi), Simiyu (ACP Blasius Chatanda), na Mwanza (SACP Wilbroad Mutafungwa) walipotembelea Kambi Kuu ya Mkandarasi wa Kampuni ya ujenzi CCECC kwenye kituo cha Seke Stesheni kilichopo Malampaka Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu ili kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live