Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makalla atangaza kiama cha Panya Road "Mtawakuta polisi au hospitali"

Makalla6 Makalla atangaza kiama cha Panya Road

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amoss Makalla amesema Mzazi mwenye Mtoto Panya Road kuanzia leo September 15, 2022 asipomuona nyumbani asihangaike akamtafute Mwanae Kituo cha Polisi au Hospitali.

RC Makalla ameyasema hayo mapema leo katika Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Zingiziwa Chanika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Makalla ametangaza kukamatwa kwa Watuhumiwa wengi katika matukio ya Tabata, Kawe na Mizumuni ambapo amesema Watuhumiwa wengi ni wale waliotoka Magerezani na kumaliza vifungo, hivyo ameiomba Mahakama kwa ambao makosa yao yanajirudiarudia hukumu yao iwe kali zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live