Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi yavamia kijiji yapora mali, fedha

16178 Pic+majambazi TanzaniaWeb

Sat, 8 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Shinyanga. Watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wamemvamia mfanyabiashara, Burugu Mahanghija (44), mkazi wa Kijiji na Kata ya Lyabukande Shinyanga vijijini na kumpora fedha taslimu na mali yenye thamani ya zaidi ya Sh3 millionI. 

Diwani wa Kata hiyo ya Lyabukande Joseph Misri, amesema baada ya kupora fedha na mali katika duka hilo, watuhumiwa hao waliwavamia wananchi wengine waliokuwa wakiangalia taarifa ya habari katika moja ya baa za eneo hilo na kuwapiga huku wakiwapora fedha na simu.

“Kelele za kuomba msaada ziliwafanya watuhumiwa hao waliokuwa na silaha kufyatua risasi hewani kutishia wananchi kabla ya kutokomea gizani,” amesema Misri.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz