Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi wawili wauawa Gongo la Mboto wakiiba mkopo wa Milioni 1

Mulirooo Majambazi wawili wauawa Gongo la Mboto wakiiba mkopo wa Milioni 1

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: Globalpublishers

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Wananchi wa maeneo ya Gongo la Mboto wamewadhibiti majambazi wawili waliokuwa na silaha ya moto baada ya kufanya tukio la uhalifu wa kupora fedha Tsh.Milioni 1.5 maeneo ya Chanika.

Hata hivyo, majambazi hao akiwemo mmoja aliyefahamika kwa jina la Kulwa walifariki dunia wakati wanapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kipigo walichokipata kutoka kwa Wananchi.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema tukio hilo limetokea Jana jioni Oktoba 26, 2022 saa 5:30 asubuhi ambapo Wahalifu hao walipora fedha hizo kutoka katika Kikundi cha kuchangiana cha Wakina Mama Chanika waliopewa fedha hizo kutoka Taasisi ya ASA.

Kamanda Muliro alisema kuwa; “Ilipofika saa 5:30 asubuhi akina mama hao wakawa wamekusanya zile fedha zikawa zimefika Milioni Moja na Laki tano wakati wamekaa wakisubiri Mtu azichukue zile pesa wakatokea Majambazi wawili wakiwa kwenye pikipiki namba MC714CLL wakatishia kwa silaha wakapora zile pesa wakaondoka.”

Chanzo: Globalpublishers