Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majambazi walioiba Milioni 7 na simu saba wauawa (+video)

Screenshot 2020 12 10 At 20.58.53 660x400.png Majambazi walioiba Milioni 7 na simu saba wauawa (+video)

Sat, 12 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kumuua jambazi mmoja na kukamata silaha mbili aina ya Mark IV na Bastola aina ya Revolver ambayo ilikuwa na risasi 9 ndani ya magazine.

Taarifa hiyo imetolewa Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, SACP Camillius Wambura, na kusema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia  Desemba 10, 2020, maeneo ya Kimara Korogwe.

“Jambazi huyo aliyekuwa na wenzake wawili waliofanikiwa kukimbia wamekuwa wakijihusisha na matukio ya uhalifu katika Jiji la Dar es Salaam na mikoa Jirani” Wambura

“Ambapo mnamo Desemba 7, 2020, majira ya saa 4:00 usiku huko maeneo ya Tabata Msimbazi walipora fedha kiasi cha Tsh 7,800,000/= na simu saba za aina mbalimbali katika duka la wakala wa huduma za kibenki na wakala wa mitandao ya simu”,  SACP Wambura.

Aidha SACP Wambura, amesema kuwa majambazi hao walifanya tukio lingine huko Kimara, siku ya Novemba 13, 2020, majira ya saa 3:00 usiku, maeneo ya Mbezi Luis, majambazi hao wapatao wanne wakiwa na silaha aina ya Bastola na Mark IV walipora kiasi cha Tsh 20,000,000/= katika duka la wakala wa benki, mitandao ya simu na bidhaa mbalimbali.

Chanzo: millardayo.com