Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majaji 11 mahakama ya Afrika kuamua mashauri 15

1995f3afdd63e366f9092a42b6deb9b3 Majaji 11 mahakama ya Afrika kuamua mashauri 15

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imesema asilimia 70 ya mashauri 15 yaliyoanza kusikilizwa na kikao cha 63 yanatoka Tanzania.

Rais wa mahakama hiyo, Imani Aboud alisema kikao hicho kilichoanza jana kinatarajiwa kumalizika Desemba 3 mwaka huu kwa kutolewa uamuzi wa mashauri hayo.

Aboud aliwaeleza waandishi wa habari jana Dar es Salaam kuwa jopo la majaji 11 kutoka nchi 11 wanachama wanaopitia mashauri hayo.

Aliwapongeza majaji wa mahakama hiyo kwa mchango wanaoutoa katika kushughulikia mashauri na kutoa uamuzi.

"Sababu kwa nini majaji wana stahili pongezi ni kutokana na uwajibikaji wao na ujasiri, sifa zinazotakiwa kwa kila mtu na taasisi ili kupima uwezo wake," alisema Aboud.

Aliwahakikishia majaji na wafanyakazi wa mahakama hiyo kuwa mahakama itaendelea kuwepo na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Aboud alisema ingawa mahakama hiyo inakabiliwa na wakati mgumu kama vile wadau wake kusitasita na upungufu wa rasilimali lakini kutokana na ushirikiano inayopata inaweza kuzikabili changamoto hizo.

Alitoa mfano wa ushirikiano ambao mahakama hiyo inaendelea kupata kuwa ni kitendo cha nchi mbili kujiunga uanachama wiki iliyopita ambazo ni Niger na Guinea Bissau.

"Ninafahamu changamoto tulizopata kutoka kwa nchi wanachama ambazo ni Benin, Ivory Coast na Tanzania lakini leo nawakaribisha tuzungumzie maeneo chanya tuliyonufaika nayo kupitia nchi hizi," alisisitiza Aboud.

Majaji hao 11 ni kutoka nchini Tanzania ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho, Congo Brazavile Makamu Mwenyekiti, Kenya, Tunisia, Cameroon, Nigeria, Algeria, Malawi, Mali, Afrika ya Kusini na Rwanda.

Chanzo: www.habarileo.co.tz